Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa wakulima wadogo wadogo bado hauthaminiki-UNCTAD

Mchango wa wakulima wadogo wadogo bado hauthaminiki-UNCTAD

Shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD limesema kuwa wakulima wadogo wadogo ni kundi ambalo halipewi kipaumbele licha ya mchango mkubwa wanaotoa kutokana na uzalishaji.

Katika ripoti ya UNCTAD kuhusu  bidhaa na maendeleo kwa mwaka 2015, shirika hilo linasema kuwa wakulima wadogowadogo ndio asilimia kubwa ya watu masikini, licha ya kwamba ndio wazalishaji wa zaidi ya asilimi 80 ya chakula duniani.

Ripoti inaainisha baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo wakulima hao katika nchi zinazoendelea hususani jinsi wanavyojumuishwa katika uchumi wa kimataifa. Wakulima hao ni waathirika wa mabadiliko ya tabia nchi , lakini pia ni watu muhimu katika kufikia njia ya maendeleo yanayojali mazingira imesema ripoti.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wakulima hawajumuishwi katika sera zenye fursa yakinifu ikiwamo hatua za kitaifa, kikanda na kimataifa. UNCTAD pia imependekeza biashara ya  kimataifa na mikataba ya uwekezaji kuhakikisha vinatoa fursa ya biashara kwa wakulima wadogowadogo.

Samuel Gayi ni mkuu wa kitengo cha bidhaa katika UNCTAD