Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi wa rais CAR waahirishwa

Uchaguzi wa rais CAR waahirishwa

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR MINUSCA umeripoti kuwa uchaguzi wa rais na wabunge uliokuwa ufanyike tarehe 27 Disemba, umehairishwa mpaka tarehe 30 mwezi huu.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa  Stéphane Dujarric ameeleza hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani mwishoni mwa wiki, akiongeza kwamba uamuzi huo umechukuliwa na Mamlaka za Kitaifa za Uchaguzi kwa ajili ya kutimiza mafunzo kwa wahudumu wa uchaguzi na kutatua baadhi ya maswala yaliyobaki.

Moja ya masuala hayo ni usambazaji wa kura ambazo zimefika mjini Bangui siku ya jumatano, MINUSCA ikiwa na wajibu wa kuzisambaza katika majimbo yote.

(SAUTI YA STEPHANE DUJARRIC)

“ "Karatasi zote za kupiga kura ya uchaguzi wa rais na wabunge zimefika kwenye mji mkuu wa Bangui siku ya jumatano  na MINUSCA itakuwa na wajibu wa kuzisambaza katika majimbo yote. » 

Aidha ameeleza kwamba utaratibu wa kusalimisha waasi wa anti-Balaka na ex-Seleka nchini humo unaendelea.