Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wazee kuneemeka Tanzania

Wazee kuneemeka Tanzania

Utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGS ukiwa umeanza katika ngazi mbalimbali baada ya kupitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mjini New York hivi karibuni, wadau wa ustawi wa jamii nchini Tanzania wameanza kutekeleza lengo namba tatu linalohusu afya bora na ustawi.

Lengo hilo pamoja na makundi mengine pia linazungumzia wazee hususani usalama wa kiafya wa kundi hilo. Asasi ya kimataifa ya Help Age International Tanzania inatekeleza lengo hili kama anavyoeleza Mkurugenzi mkazi Smart Daniel katika mahojiano na idhaa hii ambapo amezungumzia mchakato wa sheria ya wazee nchini humo.

(SAUTI DANIEL)

Amesema katika kutekeleza lengo hilo la maendeleo endelevu SDGS namba tatu ni vyema Tanzania bara ikatekeleza kile kilichofanyika visiwani Zanzibar.

(SAUTI DANIEL)