Skip to main content

Baraza la Haki za binadamu lipewe nguvu zaidi : Rais Ruecker

Baraza la Haki za binadamu lipewe nguvu zaidi : Rais Ruecker

Rais wa Baraza la Haki za Binadamu Joachim Ruecker amesema Baraza hilo linapaswa kuwa chombo cha msingi cha Umoja wa Mataifa. Amesema hayo kwenye taarifa iliyotolewa leo wakati akihitimisha muhula wake wa mwaka mmoja kama Rais wa baraza hilo.

Bwana Ruecker ameeleza kwamba majukumu ya baraza la Haki za Binadamu yameongezeka, likipaswa kukabili la changamoto mpya, na hivyo amesisitiza umuhimu wa kulipatia nguvu zaidi

Aidha ameeleza kwamba chini ya uongozi wake ufanisi wa baraza umeimarika, akimulika pia mchango wa asasi za kijamii na vyombo vya habari katika kuzungumzia mafanikio yake. Baraza la Haki za Binadamu litaadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016.