Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya Amani ya Yemen kuanza tena Januari:

Mazungumzo ya Amani ya Yemen kuanza tena Januari:

Mazungumzo ya Amani yanayodhaminiwa na Umoja wa mataifa kwa lengo la kumaliza karibu miezi tisa ya machafuko Yemen yamemalizika nchini Uswis bila muafaka.

Takriban watu 6000 wameuawa wakati majeshi ya serikali katikabiliana na waasi wa Houthi. Sasa mazungumzo hayo yamepangwa kuanza tena Januari 14 mwakani.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed amesema kuna baadhi ya hatua zimepigwa katika mazungmzo ya karibuni ingiwa muafaka rasmi haujafikiwa.

Licha ya usitishaji mapigano wa muda kutangazwa mwanzoni mwa mazungumzo , mapigano makali yameendelea kaskazini mwa nchi kati ya waasi wa Houthi na wafuasi wa serikali.

Hata hivyo mwakilishi huyo amesema bado kutaendelea kufanyika mikutano katika wiki zijazo kwa lengo la kubaini njia ambazo anatumai zitaweka msingi na usitishaji mapigano wa kudumu na kuimarisha mchkato wa Amani.