Fursa mpya za ajira zizingatiwe ili kuwa na dunia yenye usawa:UNDP
Ripoti ya maendeleo ya binadamu iliyozinduliwa leo huko Addis Ababa, Ethiopia, imetaka serikali kuchukua hatua kuhakikisha hakuna mtu anayebakizwa nyuma katika ulimwengu wa sasa unaoshuhudia mageuzi kwenye mfumo wa utendaji kazi.
Ikiwa imeandaliwa na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, ripoti hiyo imesema kasi kubwa ya maendeleo ya teknolojia, kuimarika kwa utandawazi, ongezeko la wazee na changamoto za kimazingira vinabadilli vile ambavyo watu walikuwa wanafanya kazi zamani.
Mtawala Mkuu wa UNDP Helen Clark, amesema mazingira hayo yanakuwa fursa kwa watu wengine huku wengine wakiachwa nyuma.
Kwa mantiki hiyo ametaka serikali ziweke sera ili kuhakikisha mazingira hayo yanamnufaisha kila mtu na fursa za ajira zilizopo kama vile huduma ya malezi ambayo kwa sasa inafanywa na wanawake na wengi hawalipwi ujira pamoja na ubunifu ,zinatumika kuleta tija na maendeleo endelevu.
James Wakiaga ni mshauri wa uchumi katika UNDP, Ethiopia.
(Sauti ya James)