Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM wataka utekelezaji wa muafaka wa Doha:WTO

Wataalamu wa UM wataka utekelezaji wa muafaka wa Doha:WTO

Wakati wa kuelekea mkutano wa 10 wa shirika la biashara duniani WTO ngazi ya mawaziri, kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa limetoa wito kwa serikali kote duniani kufanikisha mazungumzo ya Doha ya ajenda ya Maendeleo na sio kupuuzia ahadi za awali kabla ya kushughulikia mahitaji ya uchumi unaoendelea.

Wamesema kama biashara itafanya kazi ya haki za binadamu na maendeleo ni lazima ichangie kutambua haki ya chakula cha kutosha , kiwango cha afya kinachostahili  na kuishi katika mazingira bora. Watalaamu wamertoa kauli hiyo mbele ya washawishi wanaotarajiwa kukutana mjini Nairobi Kenya kuanzia Desemba 15-18.

Wataalamu hao wamesema hakuna sababu ya msingi ya kutotekeleza muafaka wa Doha, kwani kufanya hivyo kutakuwa na athari kubwa kwa haki za binadamu katika nchi nyingi.

Wamesisitiza kwamba wajibu wa kutekeleza haki za binadamu lazima urejerelewe katika mikataba ya biashara ya kimataifa ili kuhakikisha kwamba majadiliano na sheria za WTO vinaunga mkono juhudi za maendeleo kuondoa vyanzo vya njaa, maradhi, umasikini na kuimarisha na kulinda haki za binadamu ili kuhakikisha malengi na maendeleo endelevu yanafikiwa.