Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WESP yazinduliwa, mwelekeo wa uchumi 2016 mashaka:

WESP yazinduliwa, mwelekeo wa uchumi 2016 mashaka:

Hali ya uchumi duniani kwa mwaka huu wa 2015 iliyumba kutokana na sababu kadhaa ikiwemo kuporomoka kwa bei za bidhaa ikiwemo mafuta, kuyumba kwa thamani za fedha huku kiwango cha ukuaji kikikadiriwa kuwa ni asilimia Mbili nukta Nne.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya uchumi duniani na matarajio kwa mwaka 2016, WESP, iliyotolewa leo jijini New York, Marekani na msaidizi wa katibu Mkuu kuhusu masuala ya uchumi na kijamii, DESA, Lenni Montiel.

Amesema katika mazingira hayo, mwelekeo wa ukuaji uchumi kwa mwaka 2016 unakuwa na giza hivyo ni vyema ametaja hatua za kuchukua ili kuweza kufanikisha ajenda ya maendeleo 2030.

(Sauti ya Montiel)

“Juhudi zaidi za kisera na zilizoratibiwa zinahitajika ili kuhakikisha kuna ukuaji wa kiuchumi ambao ni madhubuti, shirikishi na endelevu, ambavyo ni muhimu katika kufanikisha ajenda 2030 ya maendeleo endelevu. Watunga sera hususan kwenye nchi zinazoendelea wanajikuta katika ugumu wa kuchagua wanapohaha kusaka mizania tete kati ya malengo ya ukuaji wa uchumi na utulivu wa kifedha.”