Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu kuhusu SDGs yabisha hodi sekondari Ihungo

Elimu kuhusu SDGs yabisha hodi sekondari Ihungo

Nchini Tanzania Umoja wa Mataifa umeendelea na kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaliyopitishwa mwezi Septemba mwaka huu na nchi wanachama kwa minajili ya kuweka ustawi wa wote ifikapo mwaka 2030.

Harakati hizo zinaendeshwa na kituo cha kituo cha habari cha Umoja huo ambapo wiki hii kimefika shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo mkoani Kagera na kuelezea malengo hayo kupitia chama cha Umoja wa Mataifa, UNA tawi la shule hiyo.

Joseph Lucian ni mratibu wa UNA shule ya sekondari Ihungo anafafanua manufaa waliyopata hadi sasa..

(Sauti ya Joseph)

Mshiriki mwingine ni Amos Mandevu, mwenyekiti wa klabu ya UNA anaelezea alichojifunza.

(Sauti ya Amos)