Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhusiano kati ya kilimo na biashara wazingatiwa na FAO na WTO

Uhusiano kati ya kilimo na biashara wazingatiwa na FAO na WTO

Shirika la Chakula na Kilimo FAO na lile la Biashara Duniani WTO yamekubaliana leo kuimarisha  ushirikiano wao ili kuboresha usalama na uhakika wa chakula.

Wakuu wa mashirika haya mawili wametangaza hayo wakati ambapo mkuu wa WTO Roberto Azevedo ametembelea makao makuu ya Fao mjini Roma hapo jana, wakisisitiza uhusiano kati ya biashara na uhakika wa chakula.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa FAO  José Graziano da Silva amezingatia kwamba usawa usipopatikana katika sekta ya kilimo, umaskini hautatokomezwa.

(Sauti ya Bwana da Silva)

Kwa upande mmoja, biashara ina jukumu muhimu zaidi katika kutimiza mahitaji yanayoongezeka ya nchi zinazokosa chakula. Kwa upande mwingine, ufunguzi zaidi wa biashara unaweza kuathiri uwezo wa wananchi kuzalisha vyakula vyao”  

Mwezi Disemba mwaka huu WTO itaitisha mkutano wa ngazi ya juu mjini Nairobi ambapo maswala ya biashara kwenye sekta ya kilimo yatajadiliwa kwa kina.