Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

SDGs kunufaisha mwanamke wa kijijini: Ban

SDGs kunufaisha mwanamke wa kijijini: Ban

Leo ni siku ya kimataifa ya mwanamke wa kijijini ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin-moon akiangazia siku hii amesema ajenda ya malengo ya maendeleo endelevu SDGS imejumuisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake mashinani.

Katika ujumbe wake kwa siku hii Ban amesema uwezeshaji kwa wanawake umelenga katika kuinua maradufu uzalishaji wa kilimo na kipato cha wazlishaji wadogowadogo husuani wanawake.

Amesema wengi wa wanawake ambao hutegemea rasilimali na kilimo kwa ajili ya ustawi wao, ni zaidi ya robo ya idadi ya watu duniani akitolea mfano wa nchi zinazoendela ambapo wanawake wa vijijini wanawakilisha takribani asilimia 43 ya nguvu kazi ya kilimo.