Skip to main content

Ban awataka wadau Libya kukamilisha mchakato wa serikali ya mkataba

Ban awataka wadau Libya kukamilisha mchakato wa serikali ya mkataba

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza wito wa nchi wanachama na mashirika ya ukanda ambayo katika mkutano wa ngazi za juu mnamo Oktoba mbili aliwataka washiriki katika majadiliano yakisiasa ya Libya kukamilisha mchakato na kusaini makubaliano kwa ajili ya muundo wa serikali ya kitaifa ya mkataba.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu inasema kuwa Ban amesema washiriki katiaktukio hilo walisisitiza kuwa makubaliano ni njia pekee  ya kumaliza mgogoro unaeondelea.

Katibu Mkuu amepongeza utashi wa kisiasa na ujasiri wa Walibya ambao wamesalia katika ahadi ya kutatua janga hilo kupitia majadiliano. Amewahamasisha kutumia fursa ya makubaliano ii kuanza kujenga upya Libya na kukabiliana na changamoto za dharura za Libya.

Ban amesema ni serikali ya makataba wa kitaifa pekee utakaowaunganisha walibya na kuwawezesha kwa usaidizi wa jumuiya ya kimataifa kukabiliana na chanagmoto hizo huku akisema anasalia katika ahadi ya kusaidia nchi hiyo na watu wake kupitia mwakilishi wake na ujumbe wa UM nchini Libya UNSMIL.