Skip to main content

Marekani kuungana na nchi zaidi ya 50 kuimarisha ulinzi wa amani- Obama

Marekani kuungana na nchi zaidi ya 50 kuimarisha ulinzi wa amani- Obama

Baada ya ufunguzi,  hotuba za mjadala wa wazi zilianza kutolewa ambapo katika hotuba yake, Rais Barrack Obama wa Marekani, ametangaza kuwa Marekani itaungana baadaye leo na nchi zaidi ya 50 katika kuzindua mkakati wa kuimarisha ulinzi wa amani.

Rais Obama amesema anatambua kuwa ni lazima jamii ya kimataifa ijitahidi zaidi katika kuimarisha uwezo wa kulinda amani kabla ya uwezo huo kuhitajika.

“Uwezo huu mpya unaweza kusaidia kuzuia mauaji ya halaiki, na kuhakikisha kuwa mikataba ya amani ni zaidi ya maneno tu kwa karatasi. Pamoja ni lazima tuimarishe uwezo wetu wa pamoja wa kuweka usalama pale ambapo utawala umesambaratika, na kuwaunga mkono wale wanaotafuta haki na amani ya kudumu”

Aidha, Obama amezungumza umuhimu wa kupatia suluhu mzozo wa Syria na kukabiliana na ISIL.

 “Pale dikteta anapowachinja makumi ya maelfu ya watu wake, hilo haliwezi kuwa tu suala la nchi moja – linaibua mateso ya wanadamu kwa kiwango ambacho kinachotuathiri sote. Kundi la kigaidi linapowachinja mateka, kuwafanya wanawake kuwa watumwa, hilo si tatizo la kiusalama la nchi moja ti- ni shambulizi kwa ubinadamu wote.”