Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ni muhimu katika kufikia maendeleo endelevu: Benki ya Dunia

Teknolojia ni muhimu katika kufikia maendeleo endelevu: Benki ya Dunia

Uunganishwaji wa kidijitali ni muhimu katika uchumi wa dunia na unaweza kutumika katika kuimarisha ushirikishwaji, kurahisisha kazi, na kuimarisha ubunifu, lakini ili kuhakikisha hili ni lazima sera sahihi ziwekwe. Hiyo ni kauli ya rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim.

Dkt. Kim amesema hayo wakati wa mkutano wa majadiliano kuhusu maendeleo katika zama za dijitali, ambapo amsema kwamba Benki ya Dunia inafanya utafiti kuhusu vipi teknolojia ya kidijitali inaweza kutumika katika malengo ya maendeleo endelevu, kwa mfano  kukabiliana na umaskini na kuimarisha ustawi.

Amesema kwamba jambo muhimu la kuzingatia ni kuhakikisha kwamba teknolojia itasaidia watu masikini zaidi duniani kwani kuna mataifa mengi ambayo teknolojia bado iko katika viwango vya chini hususan maeneo ya vijijini. Aidha idadi ya wanawake wasio na huduma ya teknolojia ni kubwa zaidi.

Amesema kwamba ripoti inasisitiza mambo mengi ikiwemo ushrikiano wa sekta binafsi na umma, akitolea mfano teknolojia nchini Somalia

Nchini Somalia soko uhuru ya simu imewezesha huduma ya pesa kupitia simu licha ya mazingira magumu. Mwaka 2014 asilimia 59 ya wasomali walilipa karo ya shule na asilimia 38 walipata malipo yao kupitia huduma ya simu”

Bwana Kim ameongeza kwamba maendelo ya kidijitali ni lazima yaende sambaba na maendeleo mengine yasiyo ya kidijitali, akitoa mfano..

Angalia mfumo wa Mpesa wa kutuma pesa, ambao ulianzishwa wakati mamilioni ya Wakenya walipata simu za mkononi, lakini hilo halingefanyika iwapo wasimamizi wangezuia soko huru ya kuwezesha mpesa kushindana na benki.”

Ameongeza kwamba ni muhimu kuwe na uwiano kati ya sekta ya habari na mawasiliano na programu za kuimarisha huduma za elimu, na uwajibikaji wa watoa huduma za umma ni muhimu.