Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miji iwajibike kulinda mazingira na uendelevu: Girardin

Miji iwajibike kulinda mazingira na uendelevu: Girardin

Miji ina wajibu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hususani katika kupunguza matumizi ya hewa ukaa kutokana na shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwamo viwanda amesema Bi  Annick Girardin ambaye ni  waziri wa Ufaransa anayeshughulikia  maendeleo na nchi zinazongumza Kifaransa Francophone.

Katika majadiliano mjini New York kuhusu namna miji inavyoweza kuwa endelevu kwa kulinda mazingira  ulioandaliwa na tasisi ya miji na mabadiliko ya tabia nchi CCFLA, waziri huyo amesema miji mingi imeahidi kupambana na maabdiiko ya tabia nchi.

Akiongea kupitia mtafsriri kwa lugha ya kingereza Bi Girardin anasema

(SAUTI GIRARDIN)

"Miji na bahari huambatana, vyote kwa pamoja vyaweza kuchangia katika uvumbuzi wa suluhu na uhusiano baina ya nchi za Kaskazini na Kusini unaimarika hususani baina ya miji katika makabiano ya mabadiliko ya tabia nchi.’’

Amesema ifikapo mwaka 20130 dunia itakuwa na idadi ya watu bilioni tano ambapo miji itakayokuwepo wakati huo bado haijajengwa hivyo ni wakati wa kupanga miji bora sasa.