Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taasisi jumuishi na zinazowajibika zitawezesha maendeleo endelevu - Mkuu wa Safaricom

Taasisi jumuishi na zinazowajibika zitawezesha maendeleo endelevu - Mkuu wa Safaricom

Mkuu wa kampuni ya Simu ya Mkononi nchini Kenya, Safaricom, Bob Collymore amesema kuna haja ya kuwepo kwa mikakati dhabiti ya kupambana na ufisadi ili kuhakikisha usawa katika jamii hususan katika upatikanaji wa haki katika muktadha ya mataifa yanayoendelea.

Collymore amesema haya wakaki wa mjadala kuhusu nafasi ya taasisi katika kufikia Ajenda ya Maendeleo Endelevu, uliofanyika katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Collymore amesema taasisi za kishera ni lazima zifanye kazi kwa pamoja, akitolea mfano wa jela, akisema hoja maalum ya jela sio tu kama taasi ya kumuadhibu mhalifu bali pia ichangie katika kumpa nuru maishani ili aweze kurejelea hali ya kawaida.

Na ili kuhakikisha taasisi zinafanya kazi kwa sababu ya wanyonge, Collymore amesema

(SAUTI 1 COLLYMORE)

"Ni lazima kuwe na ugatuzi wa taasisi ambazo kwazo kuna ufanisi wa uhakiki wa ubora  sawa na mfumo wa uwajibikaji . Huduma zinaweza kuwa na ugatuzi , lakini sera na viwango vya ubora ni lazima viwekwe na kufuatiliwa kutoka sehemu maalum ya pamoja”

Kuhusu haki, Collymore amesihi

"Haki lazima ipatikane kinadharia, kiuchumi na kilugha, na lazima iwe huru na bila upendeleo na ubaguzi. Ni lazima tuhakikishe kwamba wanawake na walio wachache wanaweza kupata haki kwa urahisi "