Taasisi ya Bunge ni muhimu katika kufikia malengo ya SDG's: IPU
Ili kufanikiwa kwa Ajenda Endelevu iliyopitishwa na viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani Ijumaa ya Septemba 25, ni lazima kuwepo kwa taasisi dhabiti, hususan bunge la kitaifa.
Ni kauli ya Rais wa Umoja wa mabunge duniani, IPU Saber Hossain Chowdhury wakati wa mjadala kuhusu kujenga taasisi mahsusi zinazoyowajibika katika kufikia malengo hayo.
Chowdhury amesema, mojawapo ya funzo kutokana na malengo ya milenia, MDG’s ni pengo kati ya kupitishwa kwa malengo na utekelezaji.
(SAUTI CHAWDHURY)
“Kama hatutabadilisha mwenendo kuhusu utekelezaji wa SDG’s, basi tutakuwa na wakati mgumu sana . Bila taasisi imara , kutakuwa na utekelezaji dhaifu, na hivyo hakutakuwa na utimizaji "
Halikadhalika Chawdhury amesema japo malengo hayo yameazimia hatma ya watu wengi, lakini ni lazima cha msingi kuwepo kwa uwajibikaji.
(SAUTI CHAWDHURY)
"Wakati tunazungumzia uwazi, sio tu ikiambatana na uwajibikaji. Tuna kwenda zaidi ya uwazi ; tunapaswa kuangazia kuwepo kwa fikra mpya "
Aidha, Rais huyo wa IPU amesihi kuwepo kwa uhusiano wa karibu kati ya bunge na ofisi ya rais, japo wakati mwingi marais hawataki kuchunguzwa.