Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya mazingira magumu, Aqeela ajitoa kwa hali na mali kumkomboa mtoto wa kike.

Licha ya mazingira magumu, Aqeela ajitoa kwa hali na mali kumkomboa mtoto wa kike.

Suala la mtu kuwa ukimbizini ni tatizo kubwa na upatikanaji wa mahitaji muhimu kama vile chakula na malazi unakuwa ni adimu. Hali inakuwa mbaya zaidi kwenye suala la elimu tena ikiwa ni mtoto wa kike hasa kwenye maeneo ambayo mila, imani na tamaduni potofu zimeshika kasi kukwamisha watoto hao kupata haki yao hiyo ya msingi. Miongoni mwa wakimbizi wanaokumbwa na hali hiyo ni wale wa Afghanistan walioko Pakistani ambako inakuwa ni shida. Hata hivyo mwalimu mmoja mkimbizi kutoka Afghanistan ameamua kufungia pazia mkwamo huo na kujitoa kwa hali na mali kusaidia watoto wakimbizi wa kike wapate elimu. Naye si mwingine bali ni Aqeela Asifi! Je amefanya nini? Ungana na Amina Hassan katika makala hii.