Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EU fanyeni uamuzi wa kijasiri kumaliza janga la wakimbizi:UNHCR

EU fanyeni uamuzi wa kijasiri kumaliza janga la wakimbizi:UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR limeeleza masikitiko yake kufuatia Umoja wa Ulaya, EU kushindwa kuafikiana kuhusu pendekezo la kuwapatia makazi wakimbizi 120,000. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Baraza la mawaziri wa Muungano wa Ulaya lilikuwa na kikao chake mjini Brussels, Ubelgiji ambako waliridhia pendekezo la awali la kuwapatia hifadhi wakimbizi ElfuArobaini pekee, UNHCR ikisema hiyo ni hatua ya kupigiwa chepuo.

Hata hivyo UNHCR imesema hatua zaidi zenye mantiki zinatakiwa kushughulikia janga la wakimbizi Ulaya hivi sasa kwani hatma ya pendekezo la kuhifadhi wakimbizi Laki Moja na elfu ishirini halikupata muafaka.

Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR Geneva.

““Tunachosema sasa, makubaliano bayana yanahitajika bila kuchelewa zaidi ili kushughulikia mahitaji ya sasa, kwani ni uamuzi jasiri kutoka kwa nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya. Kuhamishwa kwa wakimbizi zaidi ya Elfu Arobaini kunaweza kuanza katika nchi ambazo tayari zinaunga mkono mpango huo.”