Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa 70 wa Baraza kuu la UM waanza leo.

Mkutano wa 70 wa Baraza kuu la UM waanza leo.

Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza leo Jumanne kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa chini  ya Rais wake Mogens Lykketoft  kutoka Denmark.

Kikao kitaanza kwa ajenda ya kuchagua Makamu wa Rais wa Baraza hilo na kufuatia na kikao cha kilele cha kuridhia ajenda ya maendeleo endelevu, SDG kitakachoanza tarehe 25 hadi 27 mwezi huu wa Septemba jijini New York, Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa za baraza hilo, Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Pope Francis atahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 25 mwezi Septemba kabla ya mjadala mkuu wa hotuba ya viongozi wa nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa utakaonza tarehe 28 Septemba hadi Sita Oktoba 2015.