Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Polisi na wanafunzi wahatarisha msitu wa Budongo nchini Uganda

Polisi na wanafunzi wahatarisha msitu wa Budongo nchini Uganda

Wakati ambapo umuhimu wa misitu kwa mazingira na maendeleo endelevu unamulikwa kwenye kongamano la 14 la kimataifa la misitu linalofanyika mjini Durban, Afrika Kusini, hali ya misitu iliyopo Afrika Mashariki inaendelea kutia wasiwasi. Mathalani nchini Uganda, msitu wa Budongo, karibu na ziwa Albert, maghabiri mwa nchi, unahatarishwa na mafunzo ya polisi yanayofanyika humo. Kulikoni ? Ungana na John Kibego kwenye makala hii.