Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wamulika umuhimu wa redio katika kuhamasisha mabadiliko

Vijana wamulika umuhimu wa redio katika kuhamasisha mabadiliko

Wakati maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yakifanyika leo, Mkutano wa kimataifa wa Jumuiya ya watangazaji wa redio za jamii unafanyika wiki hii mjini Accra, Ghana, ambapo wawakilishi wa Mtandao wa Wanahabari Watoto wa Tanzania wameshiriki.

Wanahabari hao watoto kutoka mtanadao unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, wameshiriki kwenye mjadala maalum, wakiangazia umuhimu wa redio za jamii katika kushirikisha vijana kwenye maswala mbalimbali ya maendeleo.

Mmoja wao ni Fatma Khamis kutoka Mtandao wa Wanahabari Watoto Zanzibar

(Sauti ya FATMA)

Akiongea wakati wa uzinduzi wa mkutano huo, Bukari Tijani ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la chakula na Kilimo FAO kwa bara la Afrika amesisitiza umuhimu wa redio za jamii katika kuhamisisha jamii kuhusu maendeleo endelevu na uhakika wa chakula.