Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani ujenzi wa makazi Jerusalem

Ban alaani ujenzi wa makazi Jerusalem

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali matangazo ya kuwa Israel imepitisha ujenzi wa makazi 300 huko ukongo wa mto Magharibi eneo liitwalo Beit El pamoja na mpango wa ujenzi wa takribani nyumba 500 Mashariki mwa Jerusalem.

Taarifa ya Katibu Mkuu imesema kuwa Bwana Ban amesisitiza kuwa makazi hayo ni kinyume na sheria za kimataifa na kikwazo cha amani na kwamba hatua hiyo haiwezi kusuluhisha nia ya Israel ya kuwa na mataifa mawili.

Ameitaka nchi hiyo kurejelea tena maamuzi hayo kwa ajili ya amani na makubaliano ya mwisho .

Bwana Ban amesema pia kuwa anahuzunishwa bado na tishio la uharibifu wa kijiji kiitwacho Susiya katika eneo la ukingo wa mto Magharibi nchini Palestina kuelekea August 03 ambapo mahakama itasikiliza malalamiko ya mipango inayofanana na hiyo.

Ameongeza kuwa uharibifu wa mali binafsi ni kinyume na sheria ya kimatifa unaopaswa kuwajibisha wahusika.