Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yafikisha vifaa tiba Aden nchini Yemen

WHO yafikisha vifaa tiba Aden nchini Yemen

Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO) limefikisha misaada ya dharura mjini Aden nchini Yemen ambapo huduma za kibinadamu zimezorota kutokana na ukosefu wa amani na kutofikika kwa eneo hilo.

Taarifa ya shirika hilo inasema kuwa vifaa vya afya vilivyowasili katika malori sita ikiwa ni sehemu ya msafara wa Umoja wa Mataifa ni pamoja na tani 46.4 za madawa, na huduma za maji na kujisafi kwa ajili ya zaidi ya wanufaika 84,000 katika wilaya nane za jimboni Aden.

Katika vifaa hivyo pia vipo vya huduma za kwanza na madawa kwa ajili ya kiwewe, ugonjwa wa kuharisha, malaria na homa ya dengue.

WHO imesema kumekuwa na mlipuko wa magonjwa hayo hatua iliyosababisha kufanyika kwa majaribio ya haraka na hivyo kutoa usaidizi kwa hospitali ya Aden nchini Yemen ili kukabiliana na homa ya dengue na malaria.