Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya kijamii yataka kubadilishwa kwa mfumo wa ushuru

Mashirika ya kijamii yataka kubadilishwa kwa mfumo wa ushuru

Mashirika ya kijamii yametoa wito wa kubadilisha mfumo wa kimataifa wa ulipaji ushuru, yakiomba usawa zaidi baina ya nchi.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa jumuiya ya kimataifa ya haki ya ushuru, Dereje Alemayehu, wakati wa uzinduzi wa kongamano la mashirika ya kijamii linalofanyika mwishoni mwa wiki hii mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, kabla ya kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo.

Amesema nchi zinazoendelea haziwezi tena kukubali uongozi wa nchi zilizoendelea katika maswala ya ulipaji ushuru.

Akihojiwa na idhaa hii mjini Addis Ababa, Alvin Mosioma, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao kwa haki ya ushuru, Tax Justice Network, ambao makao yake makuu ni Nairobi, Kenya, amezingatia umuhimu wa kuimarisha ulipaji ushuru kwa nchi Afrika, hasa katika kampuni za kimataifa zinazowekeza barani humo.

(Sauti ya Alvin)

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Lakshmi Puri, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake, UN women, amesisitiza umuhimu wa kusikia sauti ya mashirika ya kijamii, ambayo yanaomba mfumo wa kiuchumi wa kimataifa ubadilishwe.