Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jaji Deschamps wa Canada kuongoza uchunguzi wa ukatili wa kingono dhidi ya watoto CAR

Jaji Deschamps wa Canada kuongoza uchunguzi wa ukatili wa kingono dhidi ya watoto CAR

Hatimaye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametangaza jopo watatu litakalopitia upya vile ambavyo chombo hicho kilishughulikia madai ya kwamba askari wa kigeno waliochini ya Umoja huo waliwafanyia ukatili wa kingono watoto huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amewaambia waandishi wa habari kuwa jopo hilo litaongozwa na Jaji wa zamani wa mahakama kuu ya Canada Marie Deschamps na wajumbe wake ni Hassan Jallow ambaye sasa ni mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa Rwanda, ICTR na Yasmin Sooka ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya haki za binadamu nchini Afrika Kusini.

Jopo litapitia upya hatua za Umoja wa Mataifa dhidi ya tuhuma hizo zinazodaiwa kufanywa na vikosi vya kijeshi ambavyo havikuwa chini ya mamlaka yake na kutathmini ufanisi wa kanuni zilizopo na kwamba..

(Sauti ya Dujarric)

Jopo litafanya kazi yake kwa uhuru na litapatiwa fursa bila kikwazo chochote kwa kumbukumbu za Umoja wa Mataifa, wafanyakazi wake na watendaji wengine wa Umoja wa Mataifa. Umoja wa Mataifa utajitahidi kuwezesha jopo hilo kukutana na watendaji wasio wa Umoja wa hu. Pamoja na hilo, yeyote ambaye anahisi ana taarifa za kupatia jopo hilo huru basi anashawishiwa kufanya hivyo kupitia anwani ya barua pepe ya nje itakayotangazwa muda mfupi ujao.”

Kazi ya jopo hilo inatarajiwa kuanza mwezi ujao wa Julai na ripoti yatarajiwa ndani ya wiki 10 ambapo Katibu Mkuu ataiweka hadharani baada ya taratibu zote kukamilika.