Skip to main content

Kenya miongoni mwa washindi wa tuzo utumishi wa umma duniani

Kenya miongoni mwa washindi wa tuzo utumishi wa umma duniani

Kenya ni miongoni mwa nchi 18 ambazo zimeshinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya kutoa huduma bunifu za umma, wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Umoja wa Mataifa ya Utumishi wa Umma.

Hafla hiyo ya kutoa tuzo itafanyika mnamo Juni 23 mjini Medellin Colombia, mwishoni mwa kongamano litakaloanza kesho Juni 23 likiwa na kauli mbiu, “Kubuni utoaji huduma za umma katika kutekeleza ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015”.

Msaidizi wa Katibu Mkuu katika idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii, UNDESA, Wu Hongbo, amesema tuzo hizo zinamulika aina nyingi za ubunifu zinazowezesha utoaji huduma bora kwa raia kote duniani na kuboresha maisha yao.

Amesema pia ni fursa ya kuonyesha mifano bora ya utoaji huduma za umma kwenye jukwaa la kimataifa.