Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Faraja ya makazi mapya yaleta nuru kwa mtoto Mwigulu.

Faraja ya makazi mapya yaleta nuru kwa mtoto Mwigulu.

Mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto, CRC unataja misingi mikuu minne ya haki za mtoto ambayo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa. Hata hivyo mwelekeo wa usimamizi wa haki hizi za mtoto kuanzia ngazi ya familia hadi taifa uko mashakani maeneo mbali mbali duniani wakati huu dunia inaposhuhudia ukatili dhidi ya watoto.

Baadhi ya matukio ya ukatili huo ni ule wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino ambayo kwayo watoto pia ni wahanga. Hofu ya kukumbwa na ukatili huo husababisha watoto kuwaficha watoto wao na hivyo kukosa haki zao za msingi, wengine hushambuliwa na kujikuta wamebakia na ulemavu wa maisha. Miongoni mwa waliokumbwa na zahma hiyo ni mtoto Mwigulu Matonange.

Je alikumbwa na nini? Ungana na Priscilla Lecomte msimulizi wetu katika makala hii.