Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zidisheni michango kwa UNRWA: Kutesa

Zidisheni michango kwa UNRWA: Kutesa

Rais wa Baraza Kuu, Sam Kutesa ameitaka jumuiya ya kimataifa kuendeleza misaada yake ili kwasaidia wakimbizi wa kipalestina ambao wanazidi kuteseka ikiwa ni matokeo ya machafuko.

Katika hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 65 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina Bwana Kutesa amesema ni muhimu wahisani wasongeshe juhudi za UNRWA za kusaidia wakimbizi kwa kuongeza kiwango cha fedha ambapo ameainisha kuwa kwa sasa shirika hilo linatoa ulinzi kwa wakimbizi zaidi yamilioni tano katika sekta kadhaa ikiwamo elimu, afya na huduma za kijamii.

Amesema kuendelea kwa vita kunaathiri ukuaji wa kiuchumi na hali ya kibinadamu katika ukanda na hivyo kuathiri moja kwa moja maisha ya raia wakimbizi wa Kipalestina.

Rais wa baraza kuu amewapongeza viongozi awafanyakazi wa UNRWA kwa moyo wao katika kutoa huduma kwa wakimbizi ambapo amesema wanafanyakazi bila kuchoka huku akitoa salamu za rambirambi kwa waliopoteza maisha wakiwa katika juhudi za kutoa huduma kwa wahitaji.

Maadhimisho ya miaka 65 ya UNRWA yamejadili maendeleo endelevu ya wakimbizi wa Kipalestina na ulinzi wa haki zao.