Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la 104 kuhusu ajira laanza Geneva

Kongamano la 104 kuhusu ajira laanza Geneva

Kongamano la 104 kuhusu ajira limeanza leo mjini Geneva, huku Guy Ryder, Mkuu wa Shirika la Ajira Duniani, ILO, akilitaja kuwa fursa ya kubuni mapendekezo ya mkakati wa kimataifa utakaobadilisha uchumi na kuufanya wote uwe rasmi.

Bwana Ryder amesema pia, kuna fursa ya kumulika jinsi biashara ndogo ndogo za kiwango wastani zinavyoweza kuendelezwa na kuwa zenye kufungua nafasi za ajira zenye hadhi.

Amesema masuala ya ajira, usawa, uendelevu, usalama wa mwanadamu, kuhamahama kwa wafanyakazi na mazungumzo ya kijamii ambayo yanatakiwa kushughulikiwa katika mkakati wa ajira siku za usoni, ni masuala muhimu kisera kwa nyakati za sasa.

“Ni masuala ambayo serikali zinakabiliana nayo kila mahali. Vile vile, ni masuala ambayo ni ya msingi katika mamlaka na majukumu ya ILO. Ni wajibu wa shirika letu kuongoza kwenye masuala haya.”