Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

 Ban akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Cyprus

 Ban akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Cyprus

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Cyprus Nicos Anastasiades.

Katika mazungumzo kati ya viongozi hao wawili, Katibu Mkuu Ban amekaribisha nia mpya ya kuanza tena kwa mazungumzo yenye nia ya kufanikisha makazi ya kudumu nchini Cyprus.

Pia wamebadilishana mawazo kuhusu mabadiliko ya tabi nchi kuelekea mkutano unaoandaliwa naUmoja wa Mataifa kuhusu sauala hilo mjini Paris mwezi Desemba mwaka huu.