Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DPRK kuna dalili njema kuhusu haki, jamii ya kimataifa iendeleze: Simonovic

DPRK kuna dalili njema kuhusu haki, jamii ya kimataifa iendeleze: Simonovic

Jamii ya kimataifa inatakiwa kuendeleza umakini wake katika kufuatialia ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea kukumba mamilioni ya watu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK.

Kauli hiyo imetolewa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu  haki za binadamu Ivan Simonovic alipozungumza mjini New York, wakati wa kikao kiliachoangazia haki za binadamu DPRK, amapo pia baadhi ya wahanga wa vitendo hivyo walitoa ushuhuda wao.

Bwana Simonovic amesema ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataiaf kwa upande wake mwezi Juni mwaka huu itafungua ofisi yake huko Seoul, Korea Kusini ambayo pamoja na mambo mengine itatoa usaidizi wenye lengo la kuboresha haki za binadamu DPRK.

Hata hivyo Simonovic amesema kwa mwaka uliopita kumekuwepo na ishara za serikali ya DPRK kujihusisha na uimarishaji wa haki ambapo..

 “Mathalani mwezi Machi mwaka huu kwa mara ya kwanza Waziri wa Mambo ya nje wa DPRK alishiriki kikao cha baraza la haki za binadamu Geneva kutetea hali ya haki za binadamu nchini mwake. Halikadhalika DPRK imeshiriki vizuri mchakato wa tathmini ya haki za binadamu. Ni lazima tuendeleze hatua hizi.”