Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Djinnit yuko Burundi kujadili hali ya ghasia iliyoibuka

Djinnit yuko Burundi kujadili hali ya ghasia iliyoibuka

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kufuatia taarifa za vifo na majeruhi vilivyotokana na ghasia za mwishoni mwa wiki nchini Burundi baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kutangazwa kuwania urais kwa awamu ya tatu.

Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari kuwa kwa sasa wanafuatilia kwa karibu hali ilivyo na kwamba ….

(Sauti ya Farhan)

“Said Djinnit, mjumbe maalum kwa maziwa makuu yuko mjini Bujumbura kuwasilisha ujumbe wa Umoja wa Mataifa na kushirikiana na pande zote husika kumaliza mvutano. Na pia tunataka uchunguzi wa haraka kuhusu ghasia hizo.”

Amesema mjumbe huyo atasisitiza wito wa awali wa Katibu Mkuu Ban Ki-moon aliotoa wakati wa mazungumzo yake ya hivi karibuni na Rais Nkurunzinza na Waziri wa Mambo ya ndani wa Burundi.