Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa elimu kwa umma chanzo cha mvutano kati ya polisi na umma:

Ukosefu wa elimu kwa umma chanzo cha mvutano kati ya polisi na umma:

Mkutano wa 13 wa kimataifa kuhusu uhalifu unaendelea huko Doha, Qatar ambako hii leo miongoni mwa mijadala iliyofanyika ni ule unaohusu marekebisho ya jeshi la polisi ikiangazia changamoto ya usimamizi wa usalama na uzingatiaji wa haki za binadamu.

Miongoni mwa waliotoa mada ni Naibu Inspekta Mkuu wa jeshi la polisi nchini Kenya, Peter Pamba ambaye ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa mjini humo sababu za kushindwa kuweka mizania kati ya mambo hayo mawili.

(Sauti ya Pamba-1) 00’19”

Na hivyo akataja vigezo wanavyozingatia kutumia nguvu…

(Sauti ya Pamba-2) 00’17”

Naibu Inspekta Mkuu huyo wa polisi amesema kwa sasa serikali ya Kenya inajitahidi kuhimiza wananchi kuzingatia sheria ili kuhakikisha usalama na kuepusha uvunjifu wa amani.