Skip to main content

Ban asikitishwa na mkwamo wa mkutano wa kusaka amani Sudan.

Ban asikitishwa na mkwamo wa mkutano wa kusaka amani Sudan.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameelezea kusikitishwa kwake na hatua ya kukwama kwa mkutano wa awali wa mazungumzo wa kusaka amani  nchini Sudan ambao ulipaswa kufanyika mjini Addis Ababa, Ethipoia ikiwa ni matokeo ya chama tawala Congress na washirika wake kutohudhuria.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Katibu Mkuu imemkariri Ban akisisitiza kuwa ujumuishwaji kamilifu, uhuru na uwazi katika majadiliano ni muhimu katika kutafufa chanzo .

Amesema kwa mantiki hiyo mkutano huo wa awali ungekuwa hatua muhimu kuelekea amani ya kudumu nchini Sudan na kutaka wadau kuendelea kuhusisha pande zote kuelekea kuitisha mjadala wa kitaifa wenye tija.

Bwana Ban amepongeza jopo kuu la utekelezaji la Umoja wa Mataifa kwa juhudi zake zisizokoma kusaka suluhu Sudan Kusini na Sudan na kuwahakikishia uungwaji mkono na ushirikiano kutika Umoja wa Mataifa.