UNHCR yashutumu LRA kwa kuteka wakimbizi wa DRC

27 Machi 2015

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeshutumu vikali kitendo cha waasi wa Lord’s Resistance Army, LRA cha kuteka nyara wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Wakimbizi hao 15 na raia mmoja wote walitekwa nyara Jumamosi wakati wakilima shamba lao lililo upande wa DRC karibu na mpaka na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Tayari 13 wameachiliwa huru na wawili bado wanashikiliwa.

UNHCR limesema kwamba baadhi ya wahanga hao wamerejea wakiwa na vidondo na mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 amenajisiwa. Wakimbizi watatu wavulana bado hawajulikani waliko ambako UNHCR imetaka wavulana hao waachiliwe huru mara moja.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter