Kupunguza maafa ni muhimu kwa ajenda ya maendeleo: Wahlström
Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu katika kupunguza majanga Margareta Wahlström amesema mkutano wa kupunguza majanga unaoendelea mjini Sendai Japan una lengo la kuandaa mkakati wa pamoja kwa ajili ya kupunguza maafa hatari baada ya mwaka 2015.
Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa kiongozi huyo amesema mkutano huo pia unakusudia kupitia mkataba uliosainiwa miaka 10 iliyopita mjini Hyogo Japan, kwa lengo la maandalizi bora kupunguza athari za maafa.
Aidha, Wahlström amesema kuwa nchi lazima zitathmini mipango ya maendeleo endelevu na jinsi ya kukabiliana mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema mwishoni mwa mkutano huo lazima kuwe na makubaliano ya pamoja ya kupunguza hatari ya maafa kwa zama za baada ya mwaka 2015 ambayo yanaenda sambasamba na ajenda ya maendeleo ya makabiliano ya mabadiliko ya tabia nchi.