Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la afya lajumuishwa kwenye udhibiti wa majanga: UNISDR

Suala la afya lajumuishwa kwenye udhibiti wa majanga: UNISDR

Harakati za kuboresha rasimu Hyogo kuhusu udhibiti wa majanga, zimepata kichocheo kipya baada ya suala la afya kujumuishwa kwenye mkakati huo wa miaka 10..

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na upunguzaji wa madhara ya majanga UNISDR, Margareta Wahlström amesema hatua hiyo inafanya rasimu hiyo kuwa imekamilika kwa asilimia 90 kwa kuwa janga la afya madhara yake ni makubwa kuliko hata tetemeko la ardhi akitolea mfano athari za milipuko kama vile Ebola, homa ya mafua ya ndege na Ukimwi.

Hata hivyo amesema changamoto za afya zinakwenda sambamba na changamoto nyingine na hivyo kuongeza uwezekano wa jamii kukumbwa na majanga kama vile umaskini na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa mantiki hiyo amesema kujumuisha afya udhibti wa majanga asilia ni muhimu kwani mara nyingi majanga asili yanapotokea harakati za kiafya huwa zinasahaulika.

Rasimu hiyo ijulikanayo pia kama HFA2 inatarajiwa kupitishwa kwenye mkutano wa tatu wa dunia wa udhibiti wa majanga utakaoanza Sendai Japan tarehe 14 mwezi ujao.