Miaka 70 baada ya Auschwitz Birkenau bado tunachukiana:Ban

28 Januari 2015

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumatano limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya wahanga wa mauaji ya Holocaust yaliyofanywa na manazi wa kijerumani miaka 70 iliyopita ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amesema kiwango kile cha mauaji kinatisha hadi leo hii.

Kambi ya Auschwitz Birkenau ambayo ilikuwa kitovu cha mauji hayo ilikombolewa na majeshi ya washiriak miaka 70 iliyopita ambapo Ban alitembelea mwaka 2013 na kuelezea washiriki wa tukio la leo kuwa alishuhudia mitambo ya mauaji ikiwemo matanuru yaliyotumika kubadili binadamu kuwa majivu.

Hata amesema licha ya siku kupita bado chuki baina ya binadamu inaendelea na kwamba....

(Sauti ya Ban)

“Bado hatujapata jawabu la sumu iliyosababisha mauaji ya kimbari miaka 70 iliyopita. Wakati huu tunapokumbuka waliopotea, na tunapotambua vitisho vya sasa, tunafahamu cha kufanya, na ni lazima tufanye pamoja. Natarajia kushirikiana nanyi kujenga mustakhbali wenye uwiano na usawa kwa wote.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter