Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twapongeza hatua ya Uholanzi kuhusu wahamiaji: Wataalamu

Twapongeza hatua ya Uholanzi kuhusu wahamiaji: Wataalamu

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wamepongeza uamuzi wa serikali ya Uholanzi wa kupatia fedha manispaa nchini humo ambazo zinapatia maeneo ya kuishi wahamiaji wasio na makazi.Uamuzi huo unawapatia haki ya maisha yenye utu wahamiaji walioko nchini humo kihalali au kinyume cha sheria, haki inayojumuisha pia chakula, mavazi na malazi.

Katika taarifa yao wataalamu hao Philip Alston wa Australia, Francois Crépeau na Leilani Farha wa Canada wamesifu Uholanzi kwa kubadili msimamo wake wa kutambua kuwa kila mtu bila kujali anaishi nchini humo kihalali au la ana haki ya kuishi maisha yenye utu.

Wamesema serikali inayowajibika inapaswa kuelekeza rasilimali zake kwenye hudumu kwa kuzingatia wajibu wake wa kimataifa kwenye haki za binadamu.

Kwa muda mrefu serikali ya Uholanzi imeukwa inakataa kuwapatia misaada wahamiaji hao ambapo Disemba mwaka jana wataalamu hao waliibua suala hilo kwa serikali hiyo na kuisihi iwapatia wahamiaji wasio na makazi usaidizi wa dharura kabla ya sikukuu ya Krismasi.