Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Duka la kinyozi na usawa wa jinsia:UNFPA

Duka la kinyozi na usawa wa jinsia:UNFPA

Harakati za kufanikisha usawa kijinsia, afya ya uzazi na hata kampeni dhidi ya Ukimwi zinachukua sura mpya kila uchao na lengo ni kuona kuwa walengwa wanafikiwa na wanafikishiwa ujumbe sahihi. Mathalani matumizi ya kinga sahihi ili kuepusha virusi vya Ukimwi kwa kutumia mipira ya kiume ni moja ya haratakati hizo. Lakini je ujumbe waweza kufikishwa vipi? UNFPA inataka kuhusisha wanaume na hivyo imebisha hodi kwenye maduka ya vinyozi ya wanaume kwani huko mijadala huwa ya wazi zaidi na haijalishi mwanaume au mvulana Je ni kwa vipi? Ungana na Assumpta Masso kwenye makala hii..