Belarus bado inakandamiza haki za binadamu: UN

24 Disemba 2014

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la haki za binadamu nchini Belarus Miklos Haraszti amesema kuwa wakati mwaka ukielekea ukiongoni hakuna dalili yoyote inayoashiria kwamba taifa limepiga hatua katika kuimarisha haki za binadamu. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Taarifa ya George)

Akielezea hali jumla ilivyo nchini humo, mjumbe huyo amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2014 Serikali ilionyesha utayari wake wa kushughulikia mambo yanayorudisha nyuma ustawi wa haki za binadamu , lakini jambo la kushangazwa ni kwamba wakati mwaka ukikaribia kukatika hakuna hatua zozote zilizichukuliwa hadi sasa.

Amesema kuwa watetezi wa haki za binadamu pamoja na waandishiwa habari wameendelea kuandamwa na vitendo vya ukandamizwaji huku wengine wakijikuta wakitupwa kororokoroni na kuteswa vikali kutokana na misimamo yao ya kutetea haki za binadamu.

Amesema kuwa   mwezi wa Disemba serikali ilipitisha sheria mpya inayobinya mitandao ya kijamii hatua ambayo ni kielelezo kingine  kwamba serikali ya Belarus haiko tayari kuruhusu kushamiri kwa haki za binadamu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud