Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili ugaidi na uhalifu unavyotishia amani duniani

Baraza la usalama(Picha ya UM/Mark Garten)

Baraza la usalama lajadili ugaidi na uhalifu unavyotishia amani duniani

Baraza la usalama leo limekuwa na kikao cha mjadala wa wazi kuhusu vitisho dhidi ya  amani na usalama wa kimataifa ikiwamo ugaidi na uhalifu unaovuka mipaka.

Majadala huo umeangazia mbinu za kukabiliana na vitisho hivyo ambavyo vimeelezwa kuwa kikwazo katika maendeleo na haki za binadamu

Akihutubia baraza hilo msadidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya siasa Jefrey Feltman amesema

(SAUTI FELTMAN)

"Ugaidi hii leo unawakilisha kiini cha tishio la salama na maani ya kimataifa . Uhalifu unaovuka mipaka unachochea ugaidi kwa fedha , silaha na usaidizi ambao unadhoofisha nchi. Katika ziara yake hivi karibuni barani Afriaka Katibu Mkuu alikumbushwa kwamba ugaidi na uhalifu unaovuka mipaka hauwezi kushughjulikwa tofauti."

Kwa upande wake mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataifa  Téte António,    amekaribisha mjadala huo akisema ugaidi na uhalifu unaovuka mipaka ni kikwazo katika utatuzi wa migogoro mbalimbali na ustawi wa bara hilo.