Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sierra Leone na UNMEER yabuni mkakati mpya kupambana na Ebola Magharibi mwa nchi

Katika harakati za kuzua maambukizi ya Ebola, WHO imepanga timu ya watu watakaofukua miili ya watu wanaohofiwa kufariki kutokanana maambukizi ya Ebola,kijiji cha Pendebu,Sierra Leone

Sierra Leone na UNMEER yabuni mkakati mpya kupambana na Ebola Magharibi mwa nchi

Katika kudhibiti ugonjwa wa homa kali ya Ebola nchini Sierra Leone, serikali kwa kushirikiana na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia dharura ya Ebola, UNMEER wameanzisha mkakati kabambe wenye lengo la kudhibiti mlipuko unaokuwa Magharibi mwa nchi hiyo.

Katika mkakati huo wahudumu wa afya huzunguka katika maeneo hayo kubaini iwapo kuna visa vipya ili wavidhibiti haraka na kuzia ueneaji wake. Maada Rogers ni Afisa Mkaguzi katika eneo la Magaribi mwa Sierra Leone.

(SAUTI MAADA)

"Hili ni eneo lenye mlundikano wa watu wengi katika jamii. Ili kutambua kisa kiomja hapa inatulazimu kuongeza ukaguzi wetu, na hiki ncicho tunachokifanya sasa. Tumeondoa wagonjwa watano hapa. Tunatembelea tena kuona ikiwa kuna visa vingine kisha tufahamu nini cha kufanya."