Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini twasihi utulivu wa siku 30 na kwa Nigeria tayari Djinnit kukutana na Rais Jonathan: Ban

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya UM, New York.

Sudan Kusini twasihi utulivu wa siku 30 na kwa Nigeria tayari Djinnit kukutana na Rais Jonathan: Ban

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Mapigano Sudan Kusini yakiendelea, nusu ya wakazi Milioni 12 wa nchi hiyo watakuwa wamekimbia makazi yao, wana njaa au wamefariki dunia ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwa waandishi wa habari mara baada ya kulipatia Baraza la Usalama taarifa ya kile alichoshuhudia Sudan Kusini wakati wa ziara yake hivi karibuni

Amesema hali ya Sudan Kusini inatia huruma msimu wa upanzi umekaribia lakini wananchi bado hawajaweza kwenda mashambani kutokana na mapigano yanayoendelea nchini mwao.

Bwana Ban amesifu jitihada za kimataifa na kikanda za kuleta utulivu nchini humo akigusia makubaliano ya mwishoni mwa wiki huko Addis Ababa ambapo sasa amesema kazi ni kwa Rais Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar kuweka tofauti zao pembeni. Katibu Mkuu akazungumzia mkutano wa usaidizi kwa Sudan Kusini utakaofanyika wiki ijayo huko Norway..

(Sauti ya Ban)

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

 “Kuepuka njaa, natoa wito wa siku 30 za utulivu, halikadhalika nimetoa wito kuwepo kwa mahakama ili kuhakikisha uwajibikaji kwa uhalifu uliotekelezwa na pande zote. Nasihi wahisani kutoa usaidizi wao wa dhati kwa mkutano ujao wa usaidizi wa kibinadamu kwa Sudan Kusini utakaofanyika Norway utakaondaliwa kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Norway tarehe 20 Mei.”

Kuhusu tukio la kutekwa nyara wanafunzi wa kike huko Nigeria, Bwana Ban amesema bado ana masikitiko makubwa na tayari mwakilishi wake maalum huko Afrika Magharibi Said Djinnit amewasili Nigeria kwa mazungumzo na Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria. Katibu Mkuu akasema..

(Sauti ya Ban)

Kitisho cha Boko Haramu siyo suala la kipeke yake, bali linahitaji sisi kuimarisha jitihada zetu za kukabiliana na ugaidi, uharamia, usafirishaji haramu wa binadamu na hata wa madawa ya kulevya. Kwenye ukanda ambao mipaka yake iko na mashaka, tunahitaji ushirikiano wa kikanda.

Katibu Mkuu amesema wakati harakati zinaendelea kuokoa watoto walio bado matekani, ni vyema kuwapatia usaidizi wa kisaikolojia na huduma za tiba dhidi ya ukatili wa kingono pamoja na usaidizi kwa familia na jamii zao.