Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaadhimisha miaka 50 ya uwekezaji katika mataifa 170

Watoto wakicheza karibu na bwawa nchni Afganistan lililojengwa kwa pamoja na FAO(Picha ya FAO)

FAO yaadhimisha miaka 50 ya uwekezaji katika mataifa 170

Shirika la chakula duniani FAO leo na kesho linaadhimisha miaka 50 ya kazi zake katika kuimarisha uwekezaji wa umma na wa kibinafsi katika mataifa yanoyoendelea.

Lengo la kitengo cha uwekezaji katika FAO ni kushirikiana na mataifa katika kutambua njia sahihi ya kuwekeza katika kilimo na katika kuchagiza maendeleo vijijini ili kupunguza umaskini.

Aidha inashrikiana na serikali moja kwa moja ili kuratibu kuwezesha, kusimamia na kutafiti kilimo na miradi ya maendeleo.

Mkurugenzi wa kitengo cha uwekezaji cha FAO, Gustavo Merino amefafanua mpango huo.

Mpango wa FAO unabaininsha  malengo matano: kupunguza uhaba wa chakula, kupunguza umaskini, kuimarisha uzalishaji, kuimarisha uzalishaji endelevu na ustahimilivu wa mimea. Malengo hayo ni muhimu kwa kukabiliana na changamoto za baadaye.”

Kitengo cha uwekezaji kilianza kazi mwaka 1967 kwa ushrikiano na benki ya dunia ambapo kwa miongo mitano kimesaidia katika uwekezaji wa dola bilioni 110 katika nchi wanachama na kufadhili miradi takriban 2000 lkatika mataifa 170.