Valerie Amos ajiuzulu, Ban ampongeza

26 Novemba 2014

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Bi. Valeri Amos ametangaza kujiuzulu katika nafasi yake.

Akiwatangazia waandishi wa habari uamuzi wa Bi Amos, naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq akimnukuu Katibu Mkuu Ban Ki Moon amesoma tamko hilo

(SAUTI FARHAN)

"Bi Amos amenifahamisha kuhusu nia yake ya kujiuzulu kama msaidizi wa Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu . Napenda kutoa shukrani zangu kuu kwa huduma yake bora kwa Umoja wa Mataifa, jamii ya misaada ya kibinadamu na wahitaji"

Farhan amesema kuwa Katibu mkuu amempongeza Bi Amos kwa uzoefu , uongozi thabiti na ushirikiano wake na wakuu wa mashirika ya kibinadamu umesaidia kupata suluhu kwa watu wanaokumbana na madhila mabaya zaidi katika maisha yao

Amesema Bi Amos ameongoza mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ya kushughulikia misaada ya kibinadamu yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia, sekta binafsi,na katika katika ofisi nyingi za majanga na mizozo.

Bi Amos ambaye ni raia wa Uingereza aliteuliwa kuwa Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kibinadamu, OCHA mwaka 2010.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter