Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugaidi na wapiganaji mamluki vyaangaziwa kwenye baraza la Usalama

UN Photo/Devra Berkowitz
Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akihutubia Baraza la Usalama. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Bi. Julie Bishop. (Picha:

Ugaidi na wapiganaji mamluki vyaangaziwa kwenye baraza la Usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi wa ngazi ya juu kuhusu ushirikiano wa kimataifa katika kudhibiti ugaidi. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Miongoni mwa waliohutubia kwenye mkutano huo uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, Julie Bishop ni Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ambaye amesema licha ya hatua zilizochukuliwa na Umoja wa Mataifa za kudhibiti vikundi vyenye misimamo mikali na wapiganaji mamluki, bado idadi yao inazidi kuongezeka akitolea mfano huko Syria na Iraq.

Amesema ni muhimu nchi wanachama kupanua wigo wa kudhibiti vitendo hivyo kwani hatua za kijeshi pekee zinakumbwa na mkwamo. Hata hivyo amesema hatua hizo ni lazima zizingatie misingi ya kimataifa ya haki za binadamu ili vita dhidi ya ugaidi isiwe chanzo cha kukiuka haki hizo.

(Sauti ya Ban)’

“Ni lazima tuendelee kufikiria kwa kina zaidi juu ya mazingira ya msingi yanayouruhusu misimamo mikali kushamiri. Hatua za kuangalia changamoto hizi kwa mtazamo wa kijeshi zimeshindwa kuzaa matunda. Wananchi wanahitaji usawa na fursa ili waweze kuishi. Wanahitaji kuhisi wanajumuishwa na serikali zao hali kadhalika wanaaminiwa na viongozi wao.”