Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yajizatiti kutokomeza ndoa za utotoni

Mkimbizi kutoka Syria mwenye umri wa miaka 14 akiwa kwenye kambi moja nchini Lebanon na ameshikilia picha ya mchumba wake. Ndoa hii ilipangwa na wazazi wake lakini mtoto huyu hakufurahishwa na kitendo hicho. (Picha: UNHCR/L.Addario)

UNHCR yajizatiti kutokomeza ndoa za utotoni

Wakati dunia ikiendelea na siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR António Guterres ameshutumu ndoa za umri mdogo akisema watapambana kutokomeza kitendo hicho.

Amesema kwa kuzingatia kuwa ndoa za utotoni zimeota mizizi, watashirikiana na wananchi, viongozi wa kijamii pamoja na waelimishaji umma na wahudumu wa afya kutokomeza kitendo hicho kinachoathiri wasichana Milioni 15 kila mwaka.

Guterres amesema baadhi ya watu huendeleza mila zao za kuozesha watoto wao katika umri mdogo hata wanapokuwa ukimbizini huku wengine wakiona ndoa hizo ni kimbilio pekee la kujikwamua kiuchumi kupitia mahari ya watoto wao.

Kwa mantiki hiyo UNHCR ka hilo limetaka serikali kutunga na kusimamia sheria zinazoharamisha kitendo hicho na kuwapatia watoto stadi za maisha sambamba na wazazi wao kupatiwa miradi ya kujikwamua kiuchumi.

Ndoa za umri mdogo zinakiuka haki za mtoto na kumnyima fursa ya kuchanua akisema kitendo hicho kimeshamiri barani Asia, Afrika na Mashariki ya Kati.