Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulizi la kigaidi Paktika, Afghanistan

Katibu Mkuu Ban Kin Moon.Picha/Un Maktba

Ban alaani shambulizi la kigaidi Paktika, Afghanistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amelaani vikali shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya raia katika jimbo la Paktika nchini Afghanistan mnamo tarehe 23, Novemba, ambalo liliwaua watu wapatao 50 na kuwajeruhi zaidi ya 60 wengine.

Katibu Mkuu amekemea kitendo hicho cha kuwashambulia wanaume, wanawake na watoto waliokuwa wanaburudika katika hafla ya michezo ya kijamii kama siyo tu ukiukwaji wa sheria ya Afghanistan na sheria ya kimataifa, lakini akakitaja kuwa uovu usiokubalika kwa ujumla. Stephane Dujarric ni msemaji wa Katibu Mkuu:

“Katibu Mkuu ameelezea rambirambi zake kwa familia za waliouawa na kujeruhiwa, na mshikamano wake thabiti na watu wa Afghanistan ambao wamekataa kutiwa uoga na vitendo kama hivi. Anatarajia waliohusika watafikishwa haraka mbele ya mkono wa sheria.”